DC AAGIZA ALIYEMTISHIA USALAMA WA MAISHA YAKE AKAMATWE

0

 

MKUU wa Mkoa wa Lindi, Zaynab Telack, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Lindi, kumkamata na kumfikisha mahakamani mfugaji anayedaiwa kumtishia maisha, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Zainabu Kawawa ili kujibu tuhuma zinazomkabili za kutishia kumuua kiongozi wa serikali.

Alitoa agizo hilo baada ya Kawawa kudai kwenye kikao cha viongozi na wafugaji, kuwa mmoja wa wafugaji amemtishia maisha baada ya kumhoji kama ameingiza mifugo wilayani humo kihalali.

Akitoa agizo hilo kwa polisi, Telak alisema haiwezekani kusikia kiongozi wa serikali aliyepewa dhamana ya kuongoza watu Kilwa, akitishiwa usalama wa maisha yake, huku yeye akiendelea kunyamaza bila ya kuchukua hatua za kisheria.

“Huyu ni kiongozi aliyepewa kazi ya kumsaidia Rais wa Tanzania kwenye wilaya, iweje anatishiwa usalama wake wa maisha tuendelee kukaa kimya, haiwezekani,” alisema Telak.

Alisema mtu au kikundi cha watu wasiotaka kutii na kuheshimu wenzao wakiwamo viongozi wa serikali mkoani Lindi, hawawezi kuachwa waendelee kutamba bila kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

“Ninakuagiza RPC hakikisha huyu mfugaji anakamatwa na kumfikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili,” alisisitiza Telak.

Alisema, amepewa dhamana ya kumsaidia rais, hawezi kukubali kuona wananchi na watumishi wa umma wanaonewa na wachache bila sababu za msingi.

Awali, Kawawa alisema siku moja akiwa katika ziara zake za kikazi vijijini, alifika eneo la Zingakibao na kukuta kundi kubwa la mifugo, hali iliyomshangaza na kutaka kufahamu uhalali wa mifugo hiyo.

Alisema alipouliza namna ya mifugo hiyo ilivyoingia ndani ya Wilaya ya Kilwa alijikuta akikumbana na vitisho vya kutaka kumuua kutoka kwa mfugaji huyo kama angeendelea kuhoji.

Kawawa alidai kuwa alimwelekeza dereva wake kuendelea na safari ya kuelekea ofisini kwake.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hadi sasa zaidi ya watu 15 wamepoteza maisha kutokana na mapigano kati ya wafugaji na wakulima, tangu serikali iruhusu wafugaji kutoka Ihefu Mbeya kwenda mikoa ya Kusini.

Chanzo:Nipashe

BADO HUJACHELEWA KUTUMIA FURSA HII YA AJIRA MTANDAO TUMIA VIDEO HII.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top