Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale (DC) mkoani Geita, Jamhuri William ameagiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi 191 ambao hawajafanya mtihani wa kidato cha pili kutokana na utoro, ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Msako huo wa nyumba kwa nyumba utaenda sambamba na kuwakamata wanafunzi watoro na kuwarudisha shuleni, huku mkuu huyo wa wilaya akieleza baadhi ya wazazi ndio chanzo cha wanafunzi kutohudhuria shuleni kutokana na kuwatumia kwenye shughuli za kiuchumi.
Akizungumza kwenye baraza la madiwani la halmashauri hiyo, William alisema Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya elimu bure, hivyo kitendo cha wanafunzi 191 kushindwa kufanya mtihani ni kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi anafanikiwa kupata elimu msingi ambayo ni darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Pia aliagiza kufanyika tathmini ya utoro kwenye madarasa ya kidato cha kwanza hadi cha nne, ili kubaini ukubwa wa tatizo na kuja na njia ya nini kifanyike kumaliza tatizo hilo.
JE! UNATAFUTA FURSA ZA AJIRA MTANDAONI?