Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe imesema kwamba diwani huyo amefariki dunia leo Novemba 16, 2022 wakati akipatiwa matibabu jijini Mbeya
"Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa masikitiko makubwa anatangaza kifo cha Diwani wa Kata ya Kinyika Mhe.Mwalyoyo kilichotokea leo tarehe 16.11.2022 jijini Mbeya.
Taratibu za mazishi zinafanywa na kwa mujibu wa wanafamilia mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18.11.2022 kijijini kwake Kinyika
Kwa niaba ya madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete natoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa Mhe. Mwalyoyo na kwamba Halmashauri inathamini na kutambua mchango wake katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata ya Kinyika na Halmashauri kwa ujumla."
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
William M.Makufwe
Mkurugenzi Makete DC.