Ni tukio ambalo limetokea wilayani Ludewa mkoani Njombe katika eneo la Ludewa kijijini kanda ya chini ambapo Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Mtafya alimaarufu kama Sumbuko (19) ambaye inasemekana amejiua kwa kunywa maji ya betri ili kukwepa shitaka la mauaji lililokuwa likimkabili
Mtendaji wa kijiji hicho Athanas Mtega amesema mnamo Novemba 14 mwaka huu kijana huyo kwa kushirikiana na mwenzake walifanya mauaji ya kijana mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Alfred kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
"Sumbuko alikuta sms za Alfred kwenye simu ya mkewe ndipo akamshirikisha rafiki yake na kuchukua jukumu la kwenda kumpiga na kumsababishia umauti, wakati wanatafutwa na polisi Sumbuko alikutwa mahali na kuzingirwa ndipo akaona amekosa mwanya wa kukimbia ikambidi anywe maji ya betri aliyokuwa amebeba kwenye chupa".
Aidha kwa upande wake mke wa marehemu huyo Angela Mhagama amekiri kuwa alikuwa na mawasiliano na kijana huyo aliyeuwawa na mumewe huku akieleza kilichotokea baada ya mumewe huyo kuona mawasiliano yao.