HERSI AWAANGUKIA MASHABIKI YANGA KUOMBA RADHI

0

 Rais wa Yanga SC Hersi Said ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu sare ya 0-0 ya Yanga SC dhidi ya Club Africain ya Tunisia ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika uliyochezwa November 2 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.


Hersi ameomba radhi mashabikiwa Yanga SC na kuwapa pole kutokana na kutopendezwa na matokeo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi maoni yao huku akiwaomba wapuuzie kauli yake inayotumika kuwakejeli mashabiki wa Yanga.

“Baada ya mchezo huo kuisha tulipata maoni ya wanachama na wapenzi wetu, sisi kama viongozi tumeyapokea kwa mikono miwili na kamati yangu ya utendaji”

“Maoni yenu ni muhimu sana katika kujenga timu yetu, kupitia hapo wapo baadhi ya watu wasioitakia mema club yetu wakitumia kauli yangu niliyoitoa wakati nazungumza na viongozi wa matawi jijini Mwanza wakiitumia kauli ile kuwakejeli baadhi ya mashabiki nataka niwahakikishie uongozi wenu umekuwa sikivu sana”

Mashabiki wa Yanga hawakuridhishwa na kiwango cha timu yao dhidi ya Club Africain kiasi cha kuamini hata mchezo wa marudiano November 9 2022 nchini Tunisia wanaenda kukamilisha ratiba.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top