IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE YAFIKIA 19...WAZIRI MKUU ATUA KAGERA

0

 Watu 19 wakiwemo abiria na wahudumu wamefariki dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Ndege la Precision Air iliyotokea asubuhi ya leo Jumapili Novemba 6, 2022.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza vifo hivyo leo jioni baada ya kuwasili kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema idadi ya Watu waliofariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea asubuhi leo Ziwa Victoria wakati ikitua imeongezeka na kufikia Watu 19.

Chalamila ametoa taarifa hiyo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la tukio Bukoba “Katika majeruhi 26 waliookolewa mwanzoni hakuna aliyefariki, maokozi ya awali yame-save Watu 26, tukaendelea kuhangaika kuokoa wengine waliobaki, Wananchi na Vyombo vya Dola, wenzetu wa redcross na magari ya Watu binafsi tumesaidiana kuivuta ndege kutoka ilipokuwa mpaka hapa iliposogea, hivi punde tumefanikiwa kuopoa miili ya Watu 19”

"Ukijumlisha Majeruhi 26 na 19 (vifo) inakuwa 45 na sio 43 tuliyoambiwa mwanzoni na kwasababu shughuli za maokozi kuna wenzetu walikuwa wanakwenda chini, tunaendelea kujiridhisha kujua kama idadi halisi ya abiria ilikuwa 43 au zaidi na kama 43 inawezekana katika maokozi haya Watu wawili ambao hawakuwa Wasafiri na wao wamepata majanga ya kupoteza maisha"

"Jitihada haizidi kudra ya Mungu, waliofariki sisi hatukupanga ni kudra za Mungu”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top