IRINGA; AJALI NYINGINE YAUA WATATU 29 WAJERUHIWA

0

 WATU watatu wamefariki duania huku wengine 29 wakiwa Majeruhi baada gari aina ya Fuso kupata ajali jana Novemba 9, 2022 katika maeneo ya Lugoda Saada Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa

Akizungumzia tukio hilo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji Mafinga, Dk. Victor Msafiri amesema kuwa jana saa 9 alasiri alipokea majeruhi 32 kati ya hao watatu wapoteza maisha wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.


Aidha Dk. Msafiri Amesema kuwa hadi sasa wamefikia majeruhi 29 ambapo wagonjwa saba hali zao siyo nzuri taratibu za kuwapa zinaendelea kwa ajili ya kuwapeleka Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

 

"Majeruhi wao wanaume wapo 25 na wanawake 4 hata wale watatu ambao wamefari walikuwa ni wanaume lakini wagonjwa wengine wanaendelea vizuri isipokuwa hao saba tuu ndio tumewapa rufaa kwa ajili ya kuwapeleka hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu Zaidi," amesema Dk Msafiri.

Kwa upande wake mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo Elia Benito amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika maeneo ya Ndolezi wakati wanaelekea Igomba ambapo gari hiyo dereva ilimshinda hali ambayo ilisabisha kutokea kwa ajali hiyo.

 

"Tulikuwa tunaelekea kwenye biashara ya mnada ndipo tulipofika maeneo ya Igomba, dereva gari ilimshinda ndio ikatokea ajali hiyo baada ya hapo sikujua nini kimetokea," amesema Benito.

Kaimu Kamanda wa Polisi Iringa, Sunday Songwe amethibisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Ni kweli ajili imetokea ni gari aina ya Fuso limekosea njia na kwenda pembeni na kupata ajali hiyo wakiwa wanatokea mnadani kwa ajili ya biashara zao," amesema Kaimu huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top