Dunia ina mengi hasa katika utafutaji kila mmoja kwa sasa anatafuta njia ya kujiingizia kipato kwa namna mbalimbali lakini hiii hatari na nusu!
Jamaa mmoja ameamua kujibadilisha muonekano
na kuonekana kama mwanamke kasha kuanza kuwapiga wanaume pesa zao waliokuwa
wakimtongoza.
Kwa mujibu wa ripoti, jamaa huyo wa makamo
amekula nauli za wengi maarufu kama 'kukula fare' huku akijifanya kuwa
mwanamke.
Huwa anajipodoa kweli kweli kiasi kwamba
wanaopenda kujiburudisha kwenye vilabu huwa hawajui kwamba ni dume hatari kama
wao!.
Kwenye uso ni wanja ambao umepakwa kwa
miondoko kweli kweli huku midomo yake ikipewa triti kweli na kuwa kama
mwanadada.
Huku wanaume wengi wakipenda kuonja tunda wanapokutana
vilabuni, jamaa huyo hujifanya kipusa mwenye tayari kuwapa wenye kiu penzi la
kupanda na kushuka. Imagine this cute woman is a man. Amekuwa akitoanisha wanaume pesa na kuwakunywa wakitaka kwenda na yeye anawatoshanisha ati ako na periods. Wanaume walioekwa box wakashanga kwani ni periods gani hizo haziishi kila siku. Wampangia and reported him to the police. Akawaiwa. pic.twitter.com/wXy0xm7vaD
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni
mmoja aliyevutiwa na simulizi na 'mrembo' huyo akisema wanaume wengi wamekuwa
wakiambulia patupu.
Sasa bwana siku za mwizi na mdanganyifu zikamfika baada ya majaa kuamua kumripoti polisi na ikabainika kuwa alikuwa mwanaume hakuwa mrembo mwenye asali tamu.