Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina moja tu la Filbert mkazi wa kijiji cha Chibingo Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita, amewashangaza wananchi wa Kijiji hicho baada ya kuvua nguo na kuanza kutembea uchi maeneo ya sokoni.
Tukio hilo limetokea Novemba 10,2022 ambapo inasemekana alikuwa akibishana na vijana wenzake endapo anaweza kutembea uchi akipewa hela ndipo akavua na kutembea uchi na kulipwa pesa hiyo kiasi cha shilingi 15,000.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Charles Mabuli amesema waliotoa pesa na yeye mwenyewe aliyetembea uchi wote wana makosa na wamedhalilisha jamii ya Chibingo ambapo tayari wamewaadhibu kwa taratibu za jamii ya hapo.
Tazama video hii kutoka ukurasa wa redio wa Stormfm