JAMAA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE KWA KIPIGO

0

Polisi katika Wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda, wamemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 47, kwa tuhuma za kumuua mke wake aliyetambuliwa kwa jina Twikirize Ronious.

Kulingana na msemaji wa polisi wa Rwenzori Magharibi Vincent Twesige, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23, aliuawa usiku wa Novemba 11, wakati wa ugomvi wa nyumbani. 


Daily Monitor inaripoti kuwa usiku huo wa tukio hilo, majirani walimsikia mshukiwa akimpiga mke wake ambaye alikuwa akiishi naye katika nyumba ya kupanga.


Ikizingatiwa kwamba wawili hao wana mazoea ya kupigana, majirani walipuuza na hawakuingilia kati lakini walibaini mnamo Novemba 12, kuwa nyumba ya wanandoa hao ilikuwa imefungwa.


Wamesema hawakushuku chochote kibaya kwani walifikiri wawili hao walikuwa wamesameheana kama kawaida na walikuwa wameenda kulima pamoja, Hata hivyo, mashaka yao yaliongezeka walipogundua kwamba nyumba hiyo ilifungwa kwa muda mrefu hali ambayo haikuwa ya kawaida. 


Majirani hao walifichua kuwa walipompigia simu mshukiwa, aliwadanganya kuwa alikuwa na Twikirize bustanini.

Mume akiri kumuua mkewe "Mnamo Novemba 15, mshukiwa alikiri kumuua mkewe na kuongeza alikuwa ndani ya nyumba na mwili wa mkewe," polisi walieleza na Jambo la ajabu katika tukio hilo ni kwamba polisi walipovamia nyumba hiyo, walimpata mshukiwa amekula sumu na alikuwa amelala kitanda kimoja na maiti ya mke wake.


Mshukiwa alipelekwa hospitalini kwa matibabu huku mwili wa mke wake ukihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kyegegwa kwa uchunguzi wa maiti.

Chanzo: TUKO.co.ke

SASA UNAWEZA KUTUMIA MUDA WAKO WA ZIADA KUTENGENEZA AJIRA MTANDAONI KAMA HIVI

NA HII NDIO FAIDA UTAKAYOTENGENEZA KWA SIKU CHACHE NDANI YA AG


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top