JELA MIAKA 142 KWA KUISHI KINYUMBA NA MWANAFUNZI

0

Mahakama ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, imemhukumu Kurwa Nkoma (21) kwenda jela miaka 142 katika kesi mbili zilizokuwa zinamkabili, akidaiwa kuishi kinyumba na wanafunzi wawili wa kike wote wakiwa na umri wa miaka 13 kama wake zake kinyume na sheria.


Katika kesi ya kwanza Jinai Namba (36) iliyotolewa hukumu Agosti 18, 2022 na Hakimu wa Mahakama hiyo Caroline Kiliwa, ikiwa na Mashtaka matatu, mshtakiwa alihukumiwa kifungo jela Miaka 70.

Katika kesi hiyo kosa la kwanza lilikuwa kutorosha mwanafunzi bila ridhaa ya wazazi wake ambalo amehukumiwa miaka 10 jela , kosa la pili ni kubaka akihukumiwa miaka 30 na kosa la tatu kubaka pia akihukumiwa miaka 30.

Hata hivyo hakimu alisema kuwa Mshtakiwa atatumikia makosa yote matatu kwa mfutano.

Katika kesi ya Pili jinai Namba 37 ya mwaka 2022 iliyotolewa hukumu Novemba 07/11/2022 na Hakimu wa Mahakama hiyo Caroline Kiliwa, ikiwa na Mashtaka manne, mshtakiwa alihukumiwa kifungo jela Miaka 72.

Katika kesi hiyo pia kosa la kwanza lilikiwa kutorosha mwanafunzi bila ridhaa ya wazazi wake ambalo amehukumiwa miaka 10 jela , kosa la pili ni kubaka akihukumiwa miaka 30 na kosa la tatu kubaka pia akihukumiwa miaka 30 na kosa la nne likiwa kumzuia mwanafunzi kwenda shule akihukumiwa miaka 2.

Katika kesi hiyo pia hakimu alisema kuwa Mshtakiwa atatumikia makosa yote manne kwa mfutano.

Kutokana na hukumu pamoja na maelezo ya hakimu ya jinsi adhabu zitakavyotumikiwa kwenye kesi zote mbili, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kila kesi.

USIPITWE NA VIDEO HII YA FURSA ZA BIASHARA MTANDAONI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top