Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu kifungo cha Miaka (3) Bruce Karistus mwenye umri wa miaka (31) Mkazi wa kijiji cha Kitelewasi kata ya Lungemba Wilayani Mufindi kwa kosa la kumchoma moto Mtoto na kumsababishia majeraha sehemu mbali mbali za mwili wake.
Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa katika shauri la jinai namba 64 la mwaka 2022.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Edward Uphoro amesema mshtakiwa ameshikiwa kwa kosa la kumchoma Mtoto na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mawili wake.
Amesema kuwa October 21 mwaka huu mshaktiwa akiwa nyumbani kwake alipewa Taarifa na mama wa muhanga aitwaye Rebeca kwamba Mtoto wao ameiba shilingi elfu 1000.
" Baada ya kupata Taarifa hizi Mshtakiwa alimchukua Mtoto na kumpeleka jikoni na kuchukua kizinga cha moto na kuanza kumchoma sehemu mbalimbali za mawili wake ikiwemo mapajani pamona na mikononi.
Uphoro ameeleza kuwa baada ya kuona hivyo mama wa muhanga alienda kutoa Taarifa kwenye uongozi wa serikali ya kijiji na baadaye mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Mafinga na alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikiri kutenda kosa hilo.
Amesema kuwa baada ya kukiri kutenda kosa hilo amefikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake ambapo alikir i na kuhukumiwa kifungo cha Miaka mitatu Jela.
Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba Mahakama hiyo impunguzieadhabu kwa Sababu ni kosa lake la kwanza na ana familia ambayo inamtegemea lakini mahakama ikatupilia mbali maombi hayo na kutoa hukumu hiyo ya kifungo cha miaka mitatu ili iwe fundisho kwa wengine.
Kesi hiyo imesimamiwa na wakiri Mwandamizi wa Serikali Twide Mangula na kutolewa hukumu na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakamani hiyo Edward Uphoro.
FAHAMU HAYA KABLA YA KUANZA KUFANYA BIASHARA MTANDAONI.