JUMUIYA YA FARAJA YETU YATOA MSAADA WA NGUO KWA FAMILIA 60 ZENYE WATOTO YATIMA 200.

Hassan Msellem
0

Jumuiya ya Faraja Yetu Kisiwani Pemba, imetoa msaada wa nguo kwa familia 60 zenye watoto yatima 200 ili kuzisaidia familia hizo kutokana na hali duni ya kimaisha walizonazo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Makamo Mwenyekiti wa jumuiya ya Faraja Yetu Riziki Mohammed Makame, amesema lengo la kutolewa kwa msaada huo ni kuwasaidia familia zenye watoto yatima ambazo zinakabiliwa na hali duni ya kimaisha ili waweze kujistiri.


Aidha, ameongeza kuwa utolewaji wa msaada huo ni miongoni mwa misaada inayotolewa na jumuiya ya Faraja Yetu katika kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum Kisiwani Pemba ikiwemo watoto yatima, wajane pamoja na watu wenye ulemavu.


Nao baadhi ya wanafamilia ambao wamepatiwa msaada huo wameishukuru jumuiya hiyo kwakuwapatia msaada huo na kuziomba jumuiya pamoja taasisi nyengine kujitokeza katika kuzisaidia familia yenye hali duni ya kimaisha ili ziweze kupata faraja.


Mrashi Haji Faki kutoka Kiwani, ni mama mwenye mtoto yatima mmoja ambaye amepatiwa msaada wa nguo.

Msaada huo wa nguo umetolewa kwa familia 60 zenye watoto yatima 200 Shehia ya Kiwani, umetolewa jumuiya ya Faraja Yetu kwa hisani ya watu wa Uingereza.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top