KAKA ATUHUMIWA KUMUUA MDOGO KWA KUMKATAKATA

0

 Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kilema Chini wilaya ya Moshi mwenye umri wa miaka 47 kwa tuhuma za kumuua ndugu yake Gasper Mbuya (36) kwa kumkata kwa kitu chenye ncha kali.


Ingawa Jeshi hilo halijaweka wazi aina ya silaha iliyotumika katika mauaji hayo, lakini taarifa kutoka katika eneo la tukio zinadai mtuhumiwa alitumia panga kumuua ndugu yake.

Kamanda wa Polisi , Simon Maigwa, amesema, Jumamosi ya Novemba 12, 2022 saa 4 asubuhi, Jeshi hilo lilipokea taarifa za kuuawa kwa mtu huyo na mwili wake kuwekwa kwenye shimo jirani na nyumba wanayoishi wawili hao.


Kulingana na taarifa hiyo, marehemu aliuawa Novemba 6, 2022 na kwamba mwili wake uligunduliwa jana Jumamosi Novemba 12, 2022 saa 4 asubuhi huku ukiwa umekatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili na baadhi ya viungo kutenganishwa kabisa na mwili.


Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa, kiini cha mauaji hayo bado hakijafamika ingawa mtuhumiwa alikiri kuhusika na upelelezi wa tukio hilo unakamishwa na Jeshi hilo na mtumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

TAZAMA VIDEO HII ITAKUSAIDIA KUTAFUTA AJIRA MTANDAONI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top