Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Abbas Kavanda ameitaka Bodi ya Maji Bonde a Pangani pamoja na wadau wengine wa mazingira kuwachukulia hatua kali za kisheria wananchi wanao vamia vyanzo vya maji na kuharibu mazingira.
Ametoa agizo hilo Novemba 15 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti 300 katika Chemchem ya Mteruo yenye uwezo wa kutoa maji lita 28 kwa sekunde iliyopo Kata ya Uru Kaskazini Kijiji cha Ongoma Kitongoji cha Mamba ambapo ameeleza kuwa licha ya elimu kutolewa ya uhifadhi wa Rasilimali za Maji bado wapo wanachujumu sheria zenye kukataza hvyo kutakiwa kuchukuliwa sheria haraka ili kunusuru mazingira.
"Sheria imetukataza kufanya shughuliza kibinadamu katika vyanzo vya maji tunatakiwa kuacha mita sitini (60) kutoka katika vyanzo vya maji hivyo hakuna kuonea watu huruma kwani wanaenda kinyume na sheria hizi lazima tuchukue hatua haraka sana,kwasasa ni mashuhuda watu wanataabika kwa mvua kukosekana lazima watu wachukuliwe sheria ili tuwe salama"alisema Kayanda.
Aliongeza kusema kuwa ikiwa vyanzo vya maji vitaharibiwa na kupotea kutasababisha janga kubwa kwa Taifa hivyo ni vema vyanzo hivyo viweze kutunzwa kwa kupandwa miti mingi na kusimamiwa ili kuleta tija.
"Tukipoteza vyanzo hivi sijui kikazi kijacho kitakuja kuishi katika mazingira gani historia inaonesha kuwa enzi za wazee wetu maji yalikuwa yakipatikana kila mahali ila kwa sasa shughuli za kibinadamu zimechangia kupunguza maji hayo na sehemu nyingine yametoweka kabisa,sasa sisi wenye jukumu la kusimamia lazima tusimamie ili yasitoweke mbele ya macho yetu watu wapande miti na ikaguliwe kwa kusimamiwa vizuri ili kufikia lengo letu" Kayanda.
Awali akisoma taarifa ya uhifadhi wa Rasilimali Za Maji hasa chemchem hivo Evancia Marshay Afisa mazingira Bonde la Pangani amesema kuwa zipo jitihada mbalimbali zilizo fanywa kutunza chemchem hiyo ili iwe endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
"Tumesimika bango moja la makatazo ya kufanyika kwa shughuli za kibinadamu,uoteshaji wa miti takribani 500 kwa kipindi cha mwezi Juni 2021 na mpaka sasa miti 200 imekuwa sawa na asilimia 40 ya miti iliyooteshwa pia tume toa elimu kuhusu utunzaji na uhifadhi wa vyanzo wa maji kwa wananchi na zoezi hili ni endelevu"alisemaMarshay.
Aidha alieleza kuwa bado zipo changamoto zinazo kabili zoezi la utunzaji wa vyanzo vya maju licha va elimu kutolewa na kwamba bado Bodi ya Maji inaendelea kuondoa changamoto hizo kwa kutoa elimu.
"Miongoni mwa migogoro iliyopo ni pamoja na migogoro ya matumizi ya maji, uvamizi wa vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za kibinadamu kama vile kilimo na ujenzi wa makazi ya kudumu, ukataji miti rafiki iliyopo katika hifadhi ya vyanzo vya maji , utupaji wataka ngumu katika vyanzo vya maji,uchepushaji holela wa maji pasipokuwa na kibali cha matumizi ya maji pamoja na watumia maji wenye vibali kutohuisha vibali vyao pindi muda wa kibali unapoisha" Marshay .
Kwa upande wa wananchi walioshiriki zoezi hilo wameiomba Bodi ya Maji Bonde la Pangani kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa Rasilimali maji hiyo muhimu kwani adha ya Maisha pasipo kuwa na maji ya Uhakika wameanza kuiona.
"Kwa kweli kwa sasa tuna taabika upatikanaji wa maji safi na salama umekuwa wa shida kwa baadhi ya maeneo mkoani Kilimanjaro na hii yote nikutokana na sisi wananchi kuwa wakaidi kwa kuharibu mazingira lla tukipewa elimu tutabadilika japo wengine ni wabishi Daniel Makoi mwananchi.
Chemchem ya Mteruo ni miongoni mwa wanzo wa maji 978 vilivyo tambuliwa katika kanzi data ya Bodi ya Maji Bonde la Pangani,vyanzo 346 vilivyopo katika Mkoa wa Kilimanjaro na wanzo 122 vilivyopo katika wilaya ya Moshi.