"KFHI" YATOA MAFUNZO KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE ULEMAVU WA UTINDIO WA UBONGO CHAKE CHAKE.

Hassan Msellem
0

Wazazi wenye watoto wenye ulemavu wameombwa kuzingatia malezi na makuzi ya watoto ili kuhakikisha watoto hao wanapata malezi bora kama watoto wengine wasio na ulemavu.


Ombi hilo limetolewa na Afisa mdhamini kutoka ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, mheshimiwa Ahmed Abuubakar Mohammed, wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya yaliyolenga malezi na makuzi ya watoto kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo huko katika ukumbi wa mikutano wa Wawi Makonyo, ambapo amesema kuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi na walezi kutokuwa tunza na kuwajali watoto wao wenye ulemavu jambo ambalo linapelekea watoto hao kukosa haki zao za msingi ikiwemo kuchanganyika pamoja na elimu.


"Wazazi wengi pamoja na wanajamii wamekuwa na tabia ya kuwadharau na kuwatenga Hawa watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo sambamba na kuwaita majina ajabu ajabu jambo ambalo sio sahihi kabisa, naomba wazazi na Jamii itambue kuwa watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo ni watoto kama watoto wengine na wanapaswa kupendwa na kutunzwa kama watoto wengine katika Jamii zetu" alisema


Ameongeza kuwa, watu wenye ulemavu wana haki sawa na wale wasio na ulemavu, hivyo basi wanapaswa kupatiwa haki hizo ipaswavyo.


"Watu wenye ulemavu ni sawa na wale wasio na ulemavu Kwa mujibu wa sheria mbali mbali na Nchi, kikanda na hata mikataba ya umoja wa Kimataifa, hivyo basi wanapaswa kutambulisa, kuthaminiwa pamoja na kupatiwa haki na stahiki zao zote ikiwemo haki ya kuchanganyikiwa na wenzao, elimu, taaluma, ndoa pamoja na Kazi na sio kuendelea kuwa na Ile dhana potofu kuwa watu wenye ulemavu wanatakiwa kusaidiwa hapana, watu wenye ulemavu wanatakiwa kuwezeshwa na sio kusaidiwa kama tulivyozoea" Afisa mdhamin Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais


Kwa upande wake, Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Chake Chake Ndugu Mwadini Juma Ali, amesema la kutoa mafunzo hayo ni uelewa mdogo juu ya dhana mzima ya ulemavu wa utindio wa ubongo na malezi bora watoto hao katika Jamii.


Aidha amesema, Kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa na Wizara ya afya Zanzibar, zinaonesha kuwa zaidi ya watoto kumi wenye ulemavu wa utindio wa ubongo huzaliwa kila mwezi sawa na asilimia 4% watoto wote wenye ulemavu Zanzibar.

Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Chake Chake Ndugu, Mwadini Juma Ali.


Akiwasilisha mada juu ya Ulemavu wa utindio wa ubongo Ndugu, Haji Ali Hamad, amesema miongoni mwa sababu zinazopelekea ulemavu wa utindio wa ubongo kwa ni pamoja na lishe duni kwa mama mjamzito, utumiaji holela wa dawa, kosa hewa, sambamba na mtoto kukwama kwenye mlango wa shingo ya kizazi.


Nao washiriki wa mafunzo hayo, wameliomba baraza la taifa la watu wenye ulemavu pamoja na jumuiya mbali mbali za watu wenye ulemavu kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili jamii iweze kuwa uelewa wa kutosha juu ya malezi na makuzi ya watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa katika mafunzo hayo ya makuzi na malezi ya watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo.


afunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Kwa kushirikiana na afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Chake Chake na kufadhiliwa na Korea friend of hope International (KFHI) tawi la Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top