Kijana Nickson Mfoi mwenye umri wa miaka 20, akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu baada ya kuamuriwa kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10) za Kitanzania au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukiri kosa la kujifanya ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania SamIA Suluhu Hassan, kwenye mtandao wa facebook.
Na, Kamara Kenyunko, michuzi TV.
Shtaka jengine ni kuwa mshtakiwa alikutwa na
hatimiliki na kutumia simu iliyo katika umiliki wa mtu mwengine bila ya kutoa
taarifa kwa mtoa huduma.
Mfoi amekiri makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Richard Kabate baada ya kuomba kukumbushiwa mashtaka yake mahakamani
hapo.
Kabla ya kusomewa adhabu yake baada ya kutiwa
hatiani, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali, Ashura Mzava,
ameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa
wengine ambao wamekuwa wakiendelea na vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao
kwa kutumizi mabaya ya mtandao kwa kutumia majina ya viongozi na hata
kuwakashifu.
Kwa upande wake mshtakiwa ameiomba mahakama
imuonee huruma kwani wakati anatenda kosa hilo hakujua kama madhara yake ni
makubwa.
Hakimu Kabate amesema, amepitia hoja za pande
zote mbili na kuongeza kuwa “Ukimzungumzia Rais
na wazi kuwa umeizungumzia Tanzania nzima, personation iliyoko katika shtaka
hili siyo ya kawaida na jina alilolitumia siyo la kawaida hivyo lazima
uadhibiwe” Alisema Kabate
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kabate amesema katika
shtaka la kwanza la kujifanya yeye ni Rais Samia Suluhu Hassan smhtakiwa anapaswa
kulipa faini ya shilingi milioni tano au kwenda jela mwaka mmoja huku pia
katika shtaka la pili anapaswa kulipa shilingi milioni tani ama kutumikia
kifungo cha mwaka mmoja gerezani.
Hata hivyo, mahakama imesema adhabu zote hizo
zitakwenda pamoja ambapo mshtakiwa anapaswa kulipa shilingi milioni kumi na
kama atashindwa basi atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.
Katika hoja za awali inadaiwa mshtakiwa alitumia
akaunti ya Facebook yenye jina la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa
kujiwasilisha kuwa yeye ni Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia, mshitakiwa huyo alikiri kwamba kati ya
Septemba, 2021 ndani ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nia ya kulaghai
uuma alijiwasilisha kama Rais Samia Suluhu Hassan kupitia akaunti yake ya
Facebook.
Aidha, mshitakiwa huyo alikutwa na laini ya simu
ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Getness Jackson kwa madai kwamba alipewa na
mtu anayesajili laini.
“Ni kweli hii akaunti ya Facebook nilikuwa
naitumia mimi, niluziwa lakini yaliyokuwa yakiendelea humo mimi siyajui na ni
kweli nilikuwa natumia simu ambayo haijasajiliwa kwa kidole change” Alidai Mfoi
Mshtakiwa pia amekiri kwamba Septemba, 2021 alikamatwa
na askari katika hoteli ya Malaika Mkoani Mwanza na alipopekuliwa alikutwa ana
miliki simu moja na laini iliyosajiliwa kwa jina la Getness Jackoson bila ya
kutoa taarifa kwa mtoa huduma, ambapo alikamatwa na Agosti 4, 2021 aliletwa
mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yake.