KIJANA WA MIAKA 23, JELA MIAKA 20 NA KULIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 1, KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 9, PEMBA.

Hassan Msellem
0

Kesi za udhalilishaji kusikilizwa kwa kasi ya 4G Plus kupitia mahakama maalumu za kupambana na kesi za udhalilishaji Zanzibar.


Usemi huo  umedhihiri kwa kesi ya kosa la ulawiti lililofanywa na kijana Massoud Khamis Mussa mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa Vikunguni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, ambaye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 pamoja na kulipa fidia ya shilingi millioni moja kwa kosa la kumlawiti Mtoto wa kiume wa miaka 9, ambapo siku 54 pekee zilitosha kusikilizwa Kwa kesi hiyo na kutolewa Kwa hukumu.


Hukumu hiyo imetolewa juzi November 15, 2022 na mahakama maalumu ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Chake Chake Pemba.


Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame, alimuambia hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, kuwa mahakama iko tayari kusikiliza hukumu, ambapo na mshitakiwa baada ya kuulizwa na hakimu Muumini juu ya kuwa tayari kusikiliza hukumu yake alijibu Yuko tayari ndipo hakimu Muumini alipoanza kusoma maelezo ya hukumu hiyo.


Idadi ya mashahidi watano (5) wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi wao mahakamani hapo, ushahidi ambao haukuwa na kona kona kama barabara ya Chake Chake Mkoani na mahakama kujiridhisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mtoto huyo.


Idadi ya mashahidi hao ni muhanga mwenyewe, Mama mzazi wa muhanga, Jirani wa muhanga, daktari pamoja na askari mpelelezi.


"Alinichukua hadi kwenye banda lake akanilaza kwenye godoro akanivua nguo akanipa mafuta katika sehemu yangu ya siri ya nyuma, Kisha nae akavua nguo nakujipaka mafuta kwenye Uume wake na kuanza kunilawiti" alisema Mtoto huyo


Kila ambaye alisikia ushahidi huo ambao ulikuwa unaotoka kinywani kwa mtoto huyo, mdomo ulibaki wazi mithili ya mdomo wa Chewa unapoona vifaranga vya Samaki.


Ushahidi uliyotolewa na mashahidi hao watano ukiwemo wa muhanga mwenyewe uliiaminisha vyakutosha mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo, licha ya mashahidi wanne ambao walitoa ushahidi mahakamani hapo kutoa ushahidi ambao walitaraji kuwa utamvua mshitakiwa joho la hatia.


Baada hakimu Muumini, kusoma maelezo ya hukumu kwa Dakika zisizopungua kumi na tano (15) pamoja na kusoma maelezo yote ya ushahidi kwa pande zote mbili, alimtia hatiani mshitakiwa na kuuomba upande wa mashtaka kusema lolote kabla ya kutoa hukumu.


Ndipo mwendesha mashtaka wa shauri hilo Ali Amour Makamae, aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kutokana kitendo hicho Cha kinyama alichomfanyia Mtoto huyo wa Miaka 9, ukizingatia kuwa mshitakiwa ana mke ambaye angeweza kutuliza matamanio yake.


"Mheshimiwa hakimu kutokana na kitendo hichi Cha kikatili kilichofanya na mshitakiwa cha kumlawiti mtoto wa miaka 9 ukizingatia kuwa mshitakiwa ana mke ambaye angeweza kutuliza matamanio yake, naiomba mahakama yako itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na Kwa wengine wenye tabia kama hii" alisema mwendesha mashtaka huyo


Mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea, na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa vile ni kosa lake la mwanzo napia ni baba wa familia ya watoto wawili ambaye nitegemezi kwa watoto hao.


"Mheshimiwa hakimu kwavile hili ni kosa langu la mwanzo na ukizingatia mimi ni baba wa familia naiomba mahakama yako inipunguzie adhabu ili niweze kwenda kuwalea watoto wangu ambao Mimi ndio tegemeo lao" alisema mshitakiwa huyo


Baada ya mahakama kupokea maombi hayo kutoka Kwa mwendesha mashtaka na mshitakiwa, alimuamuru mshitakiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 20 pamoja na kulipa ya shilingi millioni moja kwa familia ya muhanga.


"Kwa kuzingatia maombi ya upande wa mashtaka pamoja na mshitakiwa kupitia Sheria nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar, mahakama inamuhukumu ndugu Massoud Khamis Mussa mwenye umri wa miaka 25, kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 20 sambamba na kulipa fidia ya shilingi millioni moja kwa muhanga" alisikika hakimu huyo


Shauri hilo liliwasilishwa mahakamani hapo tarehe 22/09/2022, hivyo basi ni siku 54 tu zimepita kutoka shauri hilo kuwasilishwa Mahakamani hapo hadi kufikia kutolewa kwa hukumu hiyo.


Hii inamaanisha kuwa tangu kuanzishwa kwa mahakama maalumu ya makosa ya udhalilishaji Zanzibar, kesi za udhalilishaji zimekuwa zikisikilizwa na kutolewa hukumu kwa kasi ya 4G Plus ukilinganisha na awali kabla ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo, ambapo kwasasa mahakama ya maalumu ya makosa ya udhalilishaji Chake Chake imebakiwa na mashauri matatu pekee.

 

Adhabu hiyo imetewa chini ya kifungu 299 na 314 Sheria No. 7 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.


Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame, kuwa siku ya tarehe 14.09.2022 majira ya 9:00 za jioni huko Vikunguni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa alimlawiti mtoto wa kiume wa miaka 9 jina limehifadhiwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top