Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, amesema Serikali imechukua Sehemu kubwa ya mapendelezo yaliyotolewa na Wadau kuhusu mabadiliko ya Sheria ya habari hapa nchini.
Mwenyekiti huyo wa Jukwaa la Wahariri ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kwa sasa kinachosubiriwa na wadau wa habari ni matokeo ya vikao vya Serikali na wanahabari kuhusu mabadiliko Sheria hiyo ya habari nchini.
‘‘Kwa hakika sisi kama wadau wa habari tumefika hatua nzuri na hata kuwa na matumaini chanya hasa baada ya kikao cha mwisho kati ya wanahabari na serikali, wakati unaofuata ni wa serikali na hatua zake katika kuelekea mabadiliko sheria ya habari, lakini mpaka hapa tulipofika, tunaamini kuna jambo linakwenda kutokea" amesema Balile.
Hivi karibuni, Nape Nnauye ambae ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari aliwahakikishia wadau wa habari kwamba, Serikali itakamilisha mchakato wa mabadiliko ya vipengele vya sheria ya habari.
Kauli ambayo aliitoa kwenye kikao chake na wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), Novemba 21, 2022 Jijini Dar es Salaam.