Katika Kikao cha Baraza la madiwani Novemba 1, 2022 madiwani hao pia wameelezea masikitiko yao ya barabara kutengenezwa kwa vipande vifupi vifupi na kusema hali hiyo ni kama haileti tija
Osmund Idawa na Raymond Mgaya ni Baadhi ya madiwani waliotoa maoni yao kuhusu hoja ya barabara na kusema ni afadhali barabara chache zikatengenezwa kilomita nyingi kuliko kutengeneza barabara nyingi kwa vipande vidogo vidogo
Mhandisi John Kawogo kutoka ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Makete ametolea ufafanuzi huo kwa kusema fedha zinazotolewa ni kwa ajili ya matengenezo na fedha hizo zinakuja kidogo tofauti na walivyopanga kwenye bajeti hivyo wanalazimika kutumia fedha hizo kwa uchache hivyo hivyo
Kuhusu Barabara ya Lupila Kipengere ametolea ufafanuzi kuwa baada ya mkandarasi kumaliza kutengeneza barabara ya Ibaga alikwenda Luwumbu na kwa sasa amebakiwa na mradi huo wa barabara ya Lupila Kipengere hivyo atakwenda kuitengeneza barabara hiyo
Hawa Ahmad ni Mwenyekiti wa Kikao hicho ametoa Meneja wa TARURA Kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na baraza hilo huku akimtaka kutoa vipaumbele kwa barabara ambazo hazipitiki kwa kuwa sio mgeni na barabara za wilaya ya Makete
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe ameishauri TARURA kutoa zabuni kwa wakandarasi wengi badala ya mkandarasi mmoja kupewa barabara nyingi hali inayochangia matengenezo ya barabara hizo kuchelewa kuanza.
CHANZO;GREENFM