MAKATIBU WA WABUNGE MARA WATIMULIWA KIKAONI

0

 Mkuu wa Mkoa wa Mara (RC), Meja Jenerali Suleiman Mzee amewaondoa kwenye kikao cha bodi ya barabara wawakilishi sita wa wabunge wa Mkoa wa Mara kwa maelezo wabunge wa mkoa huo wamekuwa na tabia ya kutokuhudhuria vikao vingi mkoani humo.


Mkuu huyo wa mkoa amefanya maamuzi hayo leo Jumanne Novemba 29, 2022 muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao hicho ambacho kinafanyika ukumbi wa uwekezaji mjini Musoma na kusema makatibu wa wabunge sio wajumbe halali wa kikao hicho.

Amesema kwa muda mrefu wabunge wa Mkoa wa Mara wamekuwa na tabia ya kutokuhudhuria vikao ambavyo vipo kisheria jambo ambalo amedai ni dharau na kwamba halikubaliki.


"Haya ni mazoea mkoa huu una wabunge 10 wa majimbo pamoja na wale wa viti maalum, lakini wabunge mara zote hawahudhurii vikao hivi kwa hali hii hatuwezi kufika wanashindwa kuhudhuria vikao kwaajili ya maendeleo ya mkoa hii haikubaliki" amesema na kuongeza


"Mimi siwezi kumleta katibu wangu hapa aendeshe hiki kikao maana kama ni katibu hata mimi pia ninaye. Hakuna kitu kama hicho kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake na kwa yule mwenye udhuru atoe taarifa. Niwaombe wabunge waheshimu vikao hivi ambavyo vipo kisheria, kwanza vinawasaidia hata wao," amesema.soma zaidi>>>

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top