Watoto Wawili Wamekatwa Mapanga Na Mama Yao Mzazi Katika Mtaa Wa Ilolo Kata Ya Sinde Wilaya Ya Mbeya Mjini Jijini Mbeya,Tukio Hilo Limetokea Hii Leo November 23, 2022 Nyumbani Kwake Saa Tatu Asubuhi.
Kwa Mujibu Wa Baadhi Ya Mashuhuda Wanadai Kuwa Mama Huyo Alipita Na Panga Jipya Asubuhi Na Kuingia Nalo Ndani Bila Kujua Kuwa Anakwenda Kutenda Adhma Hiyo Ya Mauaji,
Ngambi Kulaba Ngambi Ni Mwenyekiti Wa Mtaa Huo Wa Ilolo Kati Amesema Kuwa Ni Tukio La kustaajabisha Ambalo Halijawahi Kutokea Katika Mtaa Wake Huo na Kusema Kuwa Asubuhi Hiyo Yeye Alikua Nyumbani Kwake Ndipo Alipofuatwa na Mwenye Nyumba Na Kuambiwa Kuwa Waende Kwake Kuna Mauaji, Na Alipofika Alikuta ni Kweli Mauji Yametokea Na Ndipo Akachukua Jukumu La Kuwapigia Polisi Haraka.
ASP Nimbwelu Mwalukasa Ni Mkuu Wa Ushirikishwaji Wa Jamiii Wilaya Ya Mbeya Mjini Lakini Pia Ni Kaimu Mkuu Wa Upelelezi Wilaya Amesema Tukio Hilo Ni Kubwa Hivyo Wananchi Wawe Watulivu Kwani Mpaka Sasa Hawajampata Mtuhumiwa wa Mauaji Ni Nani Japo Jamii Inamuhusisha Mama Mzazi.
"Kwanza Kabisa Niwape Pole, Niwape Pole Kwa Hili Tukio Ambalo Limetokea, Ni Tukio La Kusikitusha Sana, Lakini Pia Ni Tukio La Kusikitisha Sana Lakini Vilevile nichukue nafasi hii Kuwakumbusha mambo Machache, Sisi Wananchi na Sisi Kama Wanajamii Ya Mbeya tunatakiwa kuheshimu misingi ya sheria pia Tumeona Sasa hivi Kumekuwepo Na Wimbi Kubwa La Wa Watu Kujichukulia sheria Mkononi ".
Ameongeza Kuwa Mpaka Sasa Hawajampata wala Kujua ama Kuwa Na Uhakika Kuwa Ni Nani Aliyehusika Na Mauaji Hayo "Tunakwenda Kufanya Upelelezi Taarifa zote Mtakuja kuzipata baadae japo Kuna Mengi Yanasemwa tumeelewana jamani "- ASP Mwalukasa.
Chanzo.Mbeyacityfm