MAMA AWACHOMA MOTO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WANAE KISA WANAPITA MTAANI KUOMBAOMBA

0

 Mwanamke anayefahamika kwa jina Adelina Ng'olo(36) mkazi wa kijiji cha Nyombo wilayani Njombe anashikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kuwachoma moto watoto wake wawili sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kuchukizwa na kitendo chao cha kupita mitaani kuomba msaada.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mwanamke huyo alitenda ukatili kwa wanawe octoba 28 na kisha kuwafungia ndani ,kitendo ambacho kilibainiwa na jirani mmoja na kisha kuripoti katika serikali ya kijiji.

Kamanda Issa amesema mwanamke huyo alichukua uamuzi huo baada ya kuambiwa maneno na majirani kuwa ameshindwa kulea watoto wake hadi wamegeuka kuwa ombaomba.

Kufuatia kufanyika kwa ukatili huo dhidi ya waoto ,polisi Njombe imetoa rai kwa wazazi kutekeleza majukumu yao ya ulezi wa familia kwani watoto wengi wanaingia mtaani kutafuta chakula cha kwenda kinywani kwasababu ya kutelekezwa.

Makwai Barani ni mkazi wa mji wa Njombe wametoa hisia zao juu ya mkasa huo na kisha kushauri nini kifanyike ili kukomesha vitnedo hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top