Watoto wawili mmoja akiwa na umri wa mwaka mmoja na wa pili miaka mitano wamefariki dunia na mwingine mwenye umri wa miaka 7 kunusirika kifo baada ya kulishwa sumu na Mama yao mzazi aitwaye Christina Apolinali Mkazi wa Mtaa wa Shede Mkoani Kigoma kisha na yeye kunywa sumu na kuacha barua ndefu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni ), Dkt. Stanley Binagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema Watoto hao wanasadikiwa kupewa sumu ambayo ni dawa ya kuua wadudu kwenye mifugo na mimea inayoitwa Tikitiki ambayo imekorogwa na kopo la dawa liliokotwa na Askari kwenye nyumba.
Mama huyo amekunywa sumu akiwa mjamzito ambapo Dkt Binagi amesema mpaka sasa sumu haijaweza kuathiri Mtoto aliyeko tumboni na hali ya imeanza kuwa nzuri baada ya kuzimia kwa muda mrefu akiwa Hospitalini.
Baadhi ya Majirani wamesema siku za hivi karibuni walikuwa wakiona Familia ikiwa katika hali ya kawaida na kwamba hata wao wameshangazwa na tukio hilo.
Mpaka sasa Polisi Kigoma hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo licha ya taarifa za wali kueleza Mama huyo kabla ya kufanya tukio hilo la kunywa sumu aliandika barua kueleza sababu za yeye kutaka kujiua na kuua Watoto wake lakini bado Polisi hawajasema barua iliandikwa nini.
SIKIA HII KUTOKA MTANDAONI NAMNA YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI.