MASANJA AKUTWA NDANI KWAKE AMEFARIKI

0

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi 

Na Halma Khoya, Shinyanga

 


Bibi aliyefahamika kwa jina la Lucia Masanja (78) mkazi wa Kijiji Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga, amekutwa ndani kwake amefariki dunia na mwili wake ukiwa umeoza.Mwenyekiti wa kijiji cha Nduguti wilayani Shinyanga Saleh Manota akizungumza kwa njia ya simu na vyombo vya habari , amesema tukio hilo limetokea Novemba 3 mwaka huu.

Amesema taarifa za mwili wa Bibi huyo kukutwa amefariki ndani ya nyumba yake amezipata kutoka kwa wananchi, na alipofika eneo la tukio nyumbani kwa bibi huyo akakuta kuna harufu kali huku mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.

Ameeleza kuwa baada ya kuona bibi huyo amefariki, ikabidi wapige simu Polisi na walipofika ndipo ikabidi wavunje mlango na kumkuta bibi huyo akiwa ameshafariki siku nyingi na mwili wake ukitoa harufu kali huku akiwa ameshaoza.

“Tumemkuta Bibi huyu Lucia Masanja nyumbani kwake akiwa amefariki na ameoza kabisa, inaonekana alifariki siku nyingi na wananchi wamemgundua mara baada ya kusikia harufu kali ikitoka ndani ya nyumba yake,”amesema Manota.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa yupo kwenye majukumu mengine atalitolea taarifa baadae.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top