Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoni humo, ACP Janeth Magomi amesema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Kasana Masanja (25) aliuawa Novemba 8 , 2022 majira ya saa kumi alfajiri, baada ya mtuhumiwa kumuhisi kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine.
ACP Magomi amesema kuwa baada ya uchunguzi, mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi kutokana na mwili huo kuanza kuharibika.
Mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi, na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
KARIBU UTAZAME VIDEO HII JINSI YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI.