MBARONI KWA KUTUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KISU

0

 

Mwanamke mmoja kutoka eneo la Ongata Rongai amemuua mpenzi wake mwenye umri wa miaka 47, baada ya kile kinatajwa kuwa ugomvi wa familia


Jacklyn Zakayo mwenye umri wa miaka 27, alikamatwa na anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Ongata Rongai baada ya mpenzi wake, Kennedy Bitonye Oyatsi, ambaye alikuwa dereva katika Shule ya Sheria ya Kenya, kufariki wakati wa ugomvi wao ambao chanzo chake hakijabainika.


Katika taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), majirani walioshtuka, walisikia zogo lililofuatiwa na kamsa kutoka kwa nyumba ya kupanga ya wanandoa hao Jumamosi usiku, hali iliyowafanya kukimbilia eneo la tukio kumsaidia marehemu. "Walipowasili, majirani waliona damu iliyotapakaa kwenye sakafu ya nyumba na silaha ya mauaji, kisu kilichovunjika. 


Juhudi za wasamaria wema kumkimbiza Oyatsi katika hospitali iliyoko karibu ya Sinai ziliambulia patupu kwani alitangazwa kuwa amefariki alipofika," DCI alisema.


Wapelelezi wa uhalifu katika maabara ya kitaifa ya uchunguzi wa jinai ya DCI walikagua eneo la tukio na kupata silaha ya mauaji ambayo wataifanyia uchunguzi zaidi. 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top