MKE AOMBA TALAKA KISA MUMEWE KANYOA NYWELE

0

 

Mahakama moja nchini Zambia ilipigwa na butwaa baada ya mwanamke mmoja kuielezea mahakama jinsi alivyogundua mumewe wa miaka 22 ana mwanamke mwingine nyuma ya mgongo wake.


Katika taarifa hiyo ya kushangaza ambayo ilichapishwa na vyombo vya habari nchini humo, mwanamke huyo alisema kuwa alikuwa anataka talaka kwa sababu aligundua mumewe ana mwanamke wa pili na yeye hangeweza kuvumilia ndoa ya wake wawili.

Akiulizwa alijuaje kuwa mumewe ana mke wa pili, mwanamke huyo kwa jina Karen Chungu alisema kuwa siku moja alitaka kufanya mapenzi na mumewe lakini akapigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa alikuwa amenyoa nywele za sehemu za siri.

Alitaka kujua ni kwa nini mumewe aliamua kunyoa nywele za sehemu za siri bila kumjulisha na hapo ndipo mumewe alimnyamazisha.

“Siku moja nilitaka kufanya mapenzi na mume wangu, lakini nilishtuka kumkuta amenyolewa. Nilitaka kuwe na mkutano kuhusu kwa nini sehemu zake za siri ni safi, lakini aliniambia ninyamaze kuhusu hilo. Matatizo ya ndoa yetu yaliendelea kiasi cha kunifukuza nje ya nyumba na wazee walipohusika alikimbia,” Karen alieleza mahakama ya Ndola, Zambia.

Alisema kuwa tangu tukio hilo, yeye na mumewe hawakuwahi tena kushiriki mapenzi na mumewe kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa kujitetea, mwanaume huyo kwa jina Andrew Kapembwa alisema kuwa hakuwa na nia ya kuoa mke wa pili mpaka pale mkewe alipokataa kumfulia nguo na ndio maana akaamua kumletea nyumba ndogo.

“Sikuwa na nia ya kuoa mwanamke mwingine, lakini mke wangu aliacha kunifulia na kutekeleza majukumu yake. Nilioa mwanamke mwingine kwa sababu ya tabia ya mke wangu. Sijawahi kukaa nje ya nyumba yetu kwa miaka miwili. Nilifanya makosa na nimekubali. Namheshimu mke wangu. Ni mama wa watoto wangu,” alisema.

Aidha aliambia mahakama kwamba hakufanya mapenzi na mkewe kwa sababu alimkataa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top