MLINZI WA BENKI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MBEYA

0

 Mlinzi wa kampuni ya Suma JKT, Osea Kashiririka (21) amefariki dunia baada ya kujipiga risasi sehemu ya shingo kwa kutumia bunduki.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Issango amesema tukio hilo limetokea  Jumatatu Novemba 28 majira ya saa 5:30 asubuhi maeneo ya Benki ya Azania jengo la NHIF.

Issango amesema (Kashiririka) amejiua akiwa lindoni Benki ya Azania kwa kutumia silaha aina ya shot gun pump action yenye namba 00715V mali ya Suma JKT.


"Chanzo cha tukio hili bado kinachunguzwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu."Vielelezo ambavyo ni bunduki moja, risasi nne za shot gun na ganda moja la lisasi vimehifadhiwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi," amesema Issango.

Ameongeza kabla ya kutokea tukio hilo, Kashiririka akiwa na mwenzake eneo la kazi hakuonyesha dalili yeyote ambayo ingeweza kumpa shaka mwezake.

"Ulipofika muda wa tukio (marehemu) aliingia katika chumba ambacho walinzi wanakitumia kukaa na kujifungia wakati mwenzake akiwa nje akiendelea na kazi ndipo waliposikia mlio wa bunduki, hivyo hadi polisi wanafika eneo la tukio tulikuta banda hilo limefungwa,” amesema.


Amewataka viongozi wa kampuni za ulinzi kuwa makini wakati wanampa mtu silaha ili isije kuleta madhara kwa watu wengine sababu kama mtu anakuwa na msongo wa mawazo inakuwa rahisi kuleta madhara kwa wananchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top