MTOTO WA MIAKA 7 ACHOMWA VIDOLE KISA 1000

0

Mtoto mwenye umri wa miaka saba mkazi wa Kijiji Cha Kitelewasi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi amechomwa vidole vya mikononi na baba yake mlezi kwa kile kinachodaiwa kuiba shilingi 1000 aliyoenda kununulia maandazi.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Mtoto huyo anasema siku hiyo alichukua kiasi cha shilingi 1000 kwa lengo la kununulia chakula kwani asubuhi huwa hapati hata kifungua kinywa,mchana hula chakula cha kipimo lakini jioni wakati mwingine huishia tuu kuhesabu vidole na kumeza mate.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Lungemba Brightness Sambu anasema baada ya kupokea taarifa za ukatili dhidi ya mtoto huyo hatua aliyoichukua ilikuwa ni kumkamata mtekelezaji wa tukio hilo ambaye mpaka sasa tayari yupo katika mikono ya sheria.

Diwani wa Kata ya Lungemba Samwel Mwalongo anasema baada ya kufuatilia mwenendo wa malezi ya motto huyo amebaini kuwa mtoto huyo anafanyiwa vitendo vya ukatili mara nyingi huku Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lungemba Grace Fungo akilaani vikali tukio hilo

Nilipomuuliza baba mlezi wa motto huyo kuhusu umamuzi wa kumchoma vidole mtoto kisa elfu moja majibu yake ni kwamba shetani tuu ndiye aliyempa mwongozo huo huku mama wa mtoto akisalia kushangaa licha ya kubariki tukio hilo.

TAFADHALI USIPITWE NA VIDEO HII NAKUSIHI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top