Mahakama maalumu ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba, imemuhukumu kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 14 Edson Symon Shija maarufu kwa Kila MTUMISHI mwenye umri wa miaka 42, mkaazi wa Machomane Mkoa wa Kusini Pemba, kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 4.
Hukumu hiyo imetolewa November 29.2022 na hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma.
Mbele ya hakimu Muumini Ali Juma ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtka wa Serikali Zubeir Awamu Zubeir kuwa siku ya tarehe 30\09\2022 majira ya saa 2:00 za za usiku Machomane Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa alimbaka mtoto huyo.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano ambao walitoa ushahidi mahakamani hapo dhidi ya mshtakiwa na mahakama kukubaliana na upande wa mashtaka, hivyo basi kumuamuru mshitakiwa huyo kutumikia kifungo cha miaka 14.
Kwa mara ya kwanza shauri hilo lilifunguliwa Mahakamani hapo 7\10\2022.