Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limatafuta Exavel Mgogo mkazi wa Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuuwa mke wake Catherine Peter (27) kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake.
![]() |
PICHA KUTOKA MAKTABA |
Meela ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo alikimbia ambapo jeshi hilo linaendelea kumsaka.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dada wa marehemu Mary Peter amesema wakiwa shambani alifika Mume wa marehemu Exavel Mgogo ambaye ni mtuhumiwa na kufanya mazungumzo na mkewe ( marehemu) na mara baada ya kutoelewana alichukua panga alilokua ameficha na kuanza kumshambilia sehemu mbalimbali za mwili.
Mary amesema kuwa marehemu ameacha watoto watatu pia alikuwa mjamzito
Aidha Mary ameeleza kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara ndani ya familia.
KAMA HUJAWAHI KUTENGENEZA PESA MTANDAONI TUMIA NJIA HII SASA