MWALIMU AMZUIA MWANAFUNZI KUFANYA MTIHANI KWA KUMUIBIA HELA YAKE

0

 

Vijimambo duniani hasa nchini kenya kwa Afrika Mashariki havijawahi kuisha,mara hii ni kuhusu Mwalimu anayetuhumiwa kumzuia mwanafunzi kufanya mtihani eti kisa amemuibia hela.


Inaripotiwa kwamba mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibumbu, Hellen Njeri Chabari, alimzuia mwanafunzi wa Gredi ya Sita kufanya mtihani wa KPSEA.


Kulingana na mwalimu huyo, mtahiniwa huyo alimuibia KSh2,000 na kwamba hakustahili kuwa miongoni mwa wenzake waliokuwa wakifanya mtihani kutokana na utovu wa nidhamu.


Mkuu huyo wa shule alidai kuwa ili mwanafunzi huyo afanye mtihani ni lazima alipe kwanza hela aliyomuibia.


Mama wa mtahiniwa huyo, Victoria Kagendi, alisimulia namna mwalimu mkuu alivyomtusi baada ya kuandamana na mwanawe kumrejesha shuleni. 


“Binti yangu hajaenda shuleni kwa muda sasa. Mwalimu alimfukuza shuleni kwa suala hilo hilo na akaamuru kwamba angemruhusu tu kufanya mtihani jambo ambalo sasa amekanusha,” alisimulia Kagendi huku akitokwa na machozi.


Hali hiyo ilikuwa mbaya zaidi na kumlazimu Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti hiyo Bridget Wambua, kuingilia kati kumsaidia msichana huyo na kuruhusiwa kufanya karatasi ya pili.


 Wakazi wa Kibumbu walimkashifu vikali mwalimu huyo wakisema kuwa elimu ni muhimu zaidi kuliko pesa alizodai mwanafunzi huyo aliiba.

Chanzo:Tuko.co.ke

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top