MWALIMU WA SKULI MSINGI MADUNGU JELA MIAKA 14, NA KULIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI MOJA, KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAFUNZI.

Hassan Msellem
0

 

Ilikuwa asubuhi ya saa 4:15 ya tarehe 14.11.2022 anaonekana askari anayewajibika mahakamani akiwa ameongoza na mshitakiwa Ali Makame Khatib mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mwalimu wa Skuli ya msingi Madungu kwa ajili ya kusikiliza hukumu yake inayowakabili Mwalimu huyo aliyeshitakiwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi huyo.


Uso wa Mwalimu huyo ulionekana ukiwa umesawijika sana kutokana na khofu ya kinachokwenda kutokea Mahakamani hapo, huku kama kawaida yake wakati akiwa kiririni husoma sura na nyiradi mbali mbali ili Muumba wa kila kitu aweze kumsaidia na kumfanyia takhfif juu ya kesi yake hiyo.


Mwendesha mashataka wa Serikali Ali Amour Makame, alisema upande wa mashtaka uko tayari kwa ajili ya kusikiliza hukumu dhidi ya mshitakiwa huyo.


Nao mawakili wa mshitakiwa huyo ambao ni Suleiman Omar Suleiman na Massoud Mohammed Said, walisema wako tayari kusikilizwa Kwa hukumu hiyo.


Ndipo hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alipoanza kusoma maelezo ya huku hiyo kwa muda usiopungua dakika 30,  kutoka kwenye karatasi 36 zenye maelezo ya hukumu hiyo.


Kila mtu alikuwa kimya mahakamani hapo ili kunyakua kila dondoo iliyokuwa ukiwasilishwa na hakimu huyo. 


Elimu na fani ya Sheria iliyolala kichwani kwa hakimu hiyo haikutoa picha kiurahisi kutambua kuwa mshitakiwa huyo atakutwa na hatia ama laa!


Kwa kusoma ushahidi wa upande wa mlalamikaji ambao ulikuwa na mashahidi wa nne akiwemo muathirika mwenyewe Mama mzazi wa muathirika, Daktari pamoja na Askari mpelelezi.


Ambapo maelezo ya awali ya muathirika kutoka siku ya kwanza ya kusikilizwa Kwa ushahidi mahakamani hapo Kwa upande wa mashtaka hadi kufungwa kwa shauri hilo muathirika ushahidi aliyotoa muathirika (mwanafunzi) hakuweza kubadilika wala kuonekana kuwa na chembe ya khofu Wala kutetereka ikiwemo kumtambua muhusika aliyembaka sambamba na kutambua mahala na mazingira aliyotumia mshitakiwa kutekeleza kosa hilo.


"Kwa mujibu wa ushahidi uliyotolewa na muhanga mwenyewe kuanzia siku ya mwanzo wa kusikiliza shauri hili haijaonekana kutofautiana hata Nukta, ambao muhanga alisema kuwa kwa siku tofauti mshitakiwa alikuwa anamuita mwanafunzi huyo katika chumba cha maktaba, darasani na kisha kumvua nguo ya ndani, na yeye kuvua nguo kumlaza na kisha kumbaka" alisema hakimu huyo


Ushahidi uliyotewa na mama mzazi wa mtoto huyo juu ya namna alivyogundua mtoto wake kudhalilishwa, ripoti ya daktari pamoja na ushahidi wa askari mpelelezi ni vielelezo tosha vilivyoifanya mahakama hiyo kutokuwa na chembe ya shaka juu ya mshitakiwa kufanya kosa hilo.


Kutokana ushahidi uliyotolewa mahakamani hapo, mahakama ya makosa maalum ya makosa ya udhalilishaji Chake Chake imemuhukumu mshitakiwa Ali Makame Ktahib mwenye umri wa miaka 25, ambaye pia ni mwalimu wa Skuli ya msingi Madungu kutumikia chuo cha mafunzo Kwa Kipindi cha miaka 14 Mwalimu wa Skuli ya msingi Madungu Ali Makame Khatib mwenye umri wa miaka 25, pamoja na kumlipa mlalamikaji fidia ya shilingi millioni 1 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi darasa la tano mwenye umri wa miaka 11.


Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe November 14.2022 na hakiu wa mahakama hiyo muumin Ali Juma.


Akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo hakimu Muumini, amesema kuwa siku ya tarehe 12.08.2022 majira ya 11:30 za jioni huko katika Skuli ya Msingi Madungu, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11 wakati akijua kuwa kufanya hivyo ni Kosa kisheria.


Hakimu Muumini amesema, licha ya utatezi uliotolewa dhidi ya mshitakiwa huyo kwamba siku ya tukio ambayo ni tarehe 13.08.2022 mshitakiwa aliingia Skuli na kisha kuondoka lakini kitabu cha ruhusa hakikuonesha kuondoka kwa mwalimu huyo.


"Ushahidi uliyotolewa na mwalimu mkuu unasema kuwa siku ya tukio mshitakiwa aliingia kkuli na kisha kuondoka lakini kitabu cha ruhusa hakikuonesha kielelezo chochote cha mshitakiwa kuondoka Skuli" alisema hakimu Muumini


Wakati hakimu anaendelea kusoma maelezo ya hukumu hiyo mbele ya wazazi, ndugu, Jamaa pamoja na mashahidi mshitakiwa alionekana akizidisha kisomo na nyiradi mbali mbali ili aweze kunasuka katika makucha makali ya hatia huku baadhi ya muda akionekana akikosa nguvu ya kusimama na kuamua kukaa na mara kupiga magoti na kutoa ishara ya kuomba msaada kwa kila mtu ambaye anamuangalia Mahakamani hapo hata kwa waandishi wa habari.


Kwa upande wake mwendesha mashtka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Ali Amour Makame, ameiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa waalimu wengine ambao wanajukumu la kutoa haki ya elimu kwa wanafunzi wanaowafundisha pamoja na maadili mema.


"Mheshimiwa hakimu kutokana na mshitakiwa kuwa ni mtumishi wa Umma (mwalimu) na sheria za utumishi wa Umma zinamtaka mwalimu kuwafundisha wanafunzi maadili mema, malezi pamoja na kuwapatia haki yao ya msingi ya elimu naiomba Mahakama yako itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na Kwa waalimu wengine ambao wanajukumu la kulinda maadili na malezi katika Jamii" alisema mwendesha Mashtka huyo


Nao mawakili wa mshitakiwa huyo ambao ni wakali Suleiman Omar Suleiman na Massoud Mohammed, wameiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu mshitakiwa kwavile ni mtumishi wa Umma ambaye alijitolea kwa muda mrefu katika ujenzi wa taifa sambamba na kwamba hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa kama hayo.


"Mheshimiwa hakimu kama mahakama yako inavyotambua kuwa mshitakiwa ni mtumishi wa Umma ambaye anajitolea katika ujenzi wa taifa kwa muda mrefu ukizingatia kwamba hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai tunaiomba mahakama yako kumpunguzia adhabu mshitakiwa napia ukizingatia ana wazazi ambao ni watu wazima huku wakiwa wanakabiliwa na maradhi ya presha" wakili Massoud Mohammed


Kutoka na utetezi uliyotolewa na mawakili wa mshitakiwa mahakama imekubali utetezi huo na badala ya kifungo cha miaka 30 ambapo kawaida kutolewa kwa washtakiwa wanaotiwa hatiani kwa makosa ya udhalilishaji, hivyo basi mahakama imemuhukumu mshitakiwa kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka 14.


Mashahidi watano kwa upande wa mshitakiwa walitoa ushahidi wao mahakamani hapo ingawa ushahidi huo haukuweza kumnasua mshitakiwa kutoka kwenye makucha ya hatia.


Miongoni mwa mashahidi kwa upande wa mshitakiwa ni mshitakiwa mwenyewe, Mwalimu mkuu wa Skuli ya msingi Madungu, Jirani wa karibu wa mshitakiwa, Mlinzi wa Skuli ya Madungu na mwalimu wa Skuli ya msingi Madungu.


Haki ya rufaa imetolewa kwa upande ambao haukuridhishwa na hukumu hiyo.


Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza shauri hilo liliwasilishwa mahakamani hapo August 5, 2022.


Hii ni kesi ya mwanzo Kwa mwaka 2022 inayomuhusisha mtumishi wa Serikali kwa upande wa sekta ya elimu kukutwa na hatia ya makosa ya udhalilishaji na kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 na kulipa faini ya shilingi milioni moja za Kitanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top