NYOKA ZINATUNG'ATA TUNAOMBA SERIKALI ITULETEE DAWA

0

 Katika hali isiyo ya kawaida, wananchi wa Mtwara wamelalamikia kung’atwa na nyoka wenye sumu kali huku wakiomba Wizara ya Afya kuwaletea dawa zitakazo wasaidia kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini.


Akizungumzia kadhia hiyo, Mohamed Mnaka, mkazi wa kijiji cha Nalingu kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara amesema hali kwa sasa katika maeneo ya nalingu sio nzuri.

“Hali si nzuri hapa wiki iliyopita tumezika mtu mmoja kwa kung’atwa na nyoka, hili kwetu ni tatizo kubwa tena wana sumu kali lakini hatuna dawa ya nyoka kwenye zahanati wala vituo vya afya. Hatujui kwanini, hii hutufanya tusafiri umbali mrefu ili kupata huduma ya matibabu.


“Hili jambo ni la miaka mingi, tumeishi nalo hadi sasa tunalazimika kuiomba serikali ili kulitatua, tumelia kwa miaka mingi, tunalalamika kwa miaka mingi. Hii ni hatari kwetu, tunaomba watunusuru.

“Zamani watu walikuwa waking’atwa na nyoka wanaweka mawe, kwetu yalikuwa hayasaidii, tulikuwa tunatembea na visu ukingatwa unachukua kisu unakata eneo ambalo limeathirika,” alisema Mnaka.

Diwani wa viti maalum (CCM), Mariam Lilepe ameiomba Wizara ya Afya kupeleka dawa za nyoka katika vituo vya afya na zahanati za kata za Ziwani, Madimba, Tangazo, Mahurunga, Namgogori na Kisiwa kwa dharula ili kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo wanapong’atwa na nyoka.

“Kuna wakati tuliwahi kuomba dawa tukapewa na mafanikio yalionekana lakini sasa zimeisha muda mrefu hivyo wananchi wanakosa huduma na nyoka wamekuwa wengi jamnbo ambalo linasababisha waogope kwenda mashambani kwa kuhofia usalama wao.

Kwa upande wake, mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara, Ahmed Nyembea amesema amepokea taarifa hizo na atazifuatilia ili ajue ukubwa wa tatizo.

“Ni vema watu wakipata matatizo ya kung’atwa na nyoka wawahi hospitali, yapo mambo mengi ambayo madaktari wanaweza kuyaokoa mapema kabla sumu haijasambaa mwilini,” alisema Nyembea.


Chanzo;Mwananchi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top