RAIS MWINYI ATAJA VIPAUMBELE 4, KATIKA SERIKALI YAKE, 2022-2025.

Hassan Msellem
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Hussein Ali Hassan Mwinyi, ametaja viumbe vyake kutika kipindi cha miaka miwili kutoka 2022-2025 ili kuhakikisha anatimiza ahadi zote alizotoa kwa wananchi kipindi cha kampeni na baada ya kushika madara ya kuiongoza Zanzibar.



Rais Mwinyi, ametaja vipaumbele hivyo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika kusherehekea miaka miwili ya utumishi wake katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Vipaumbele hivyo ni:-


1. Ujenzi na kuimarisha miundombinu ya Barabara, Bandari, Viwanja vya ndege sambamba na uhakika wa nishati ya Umeme na Maji.


2. Uwekezaji, hii pamoja na kokodisha visiwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji wa utalii, maeneo huru pamoja na yale yanayohiyaji kuendelezwa.


3. Kuwawezesha wananchi kiuchumi, kwa kutenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya mikopo kwa Makundi ya vijana, akina mama na wajasiriamali sambamba na kuzalisha ajira laki tatu kwa kuanzisha viwanda pamoja na vijana kujiajiri.


4. Utawala bora, kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya upinzani na kutengeneza Serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo imeleta manufaa makubwa wa wananchi wa Zanzibar.


Aidha, Dkt. Mwinyi ameahidi kuongeza idadi ya mawaziri wanawake kutokana na mawaziri wanawake kufanya vizuri zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top