Akizungumza kuhusu tatizo hilo Makoi amewataka watumishi wa Idara ya Afya kuimarisha usimamizi wa utoaji wa vibali vya kusafirisha wanyama, kukagua na kusimamia mabucha kwani kuna wafanyabiashara wanaweka nyama ya ng’ombe yenye mihuri mbele ya mabucha huku ndani wakiweka vibudu.
Idara ya Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi imesema operesheni ya kukagua mabucha ya nyama ili kubaini wafanyabiashara wanaouza nyama ya mbwa tayari imeanza huku Mganga Mkuu wa Halmashauri, Alex Kazula akibainisha kuwa wameanza kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa na tatizo hilo ikiwemo Kata ya Kibosho Kati, Okaoni na Kirima.
Naye Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kulwa Mmbando ameomba wananchi kupewa elimu ya kutonunua nyama ovyo kwa kuwa ulaji wa nyama za mbwa na ambazo hazijakaguliwa unaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUTENGENEZA $30 KWA SIKU 15 TU KUPITIA SIMU