Watu watatu wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya Ndege iliyotokea leo ziwa Victoria Mkoani Kagera ,watu 27 wakiokolewa na wengine 16 mpaka Saa kumi jioni taarifa zilizotolewa na mamlaka zimeeleza kuwa bado walikuwa wakiendelea kuokolewa kutoka kwenye Ndege hiyo.
Ndege ya Precision Air ATR 42
yenye namba za usajili 5H BWF ilianguka majini ikitokea Dar es Salaam
kuelekea Bukoba kupitia Mwanza leo asubuhi ikiwa na watu 43 (Wakubwa 38 na Mtoto mmoja) na Wafanyakazi wanne .
Baadhi ya mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo akiwemo wamesema Ndege hiyo ilipoteza uelekeo kabla ya
kutua uwanja wa Ndege.
INSERT;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;KAGERA
1
upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Albert Chalamila amesema kutokana na ajali hiyo
Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kufika mkoani
Kagera ili kuungana na timu ya ukozi.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt. Issessanda
Kaniki amethibitisha kupokea miili ya watu watatu waliofariki Dunia katika
ajali ya Ndege iliyotokea mapema Asubuhi ya Leo.
Dkt. Kaniki amebainisha kuwa wamepokea watu 26
wakiwa Hai ambapo kati yao Wanaume 17, Wanawake 9, huku Wanaume 2 na Mwanamke 1
wakipokelewa wakiwa wamefariki dunia
Uongozi wa Shirika la Ndege la Precision Air
kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Patrick Mwanri umetoa taarifa kuhusu
ajali ya Ndege yao iliyotokea Bukoba mkoani Kagera leo asubuhi wakati ikitua na
kusema watashirikiana na familia za wahanga wa ajali hiyo kwa kila hatua.
Mwanri amewaomba waandishi wa habari kutoe taarifa
sahihi ili kutopotosha umma kuhusu ajali hiyo kwani bado wanaendelea na uokozi
wa watu wengine waliokwamba kwenye ndege.
Kwa upande wa
Taarifa iliyotolewa na ENzalayaimisi Msemaji wa jeshi la Zima moto na uokoaji
makao makuu Dodoma imesema kuwa mpaka majira ya saa kumi jioni Abiria 27
walikuwa wameokolewa,watatu wakipoteza maisha na juhudi za uokozi watu 16
waliokwama kwenye ndege zilikuwa zikiendelea
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa
masikitiko taarifa ya ajali ya ndege ya Shirika la Precision katika Ziwa
Victoria, mkoani Kagera.
Rais Samia ametuma salamu za pole kwa wote
walioathirika na ajali hiyo huku akiwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu
wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya
ndege ya Shirika la Precision katika Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Natuma
salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii. Tuendelee kuwa watulivu
wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu
atusaidie. - Rais Samia Suluhu Hassan
Precision Air ndiyo shirika kubwa
la ndege la binafsi la Tanzania na kwa sehemu inamilikiwa na Kenya Airways.
Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.