TASAF MAKETE KUANZA KUWATAMBUA WATU WENYE ULEMAVU KUTOKA KAYA MASIKINI

0

 

Mpango wa kunusuru Kaya maskini TASAF Wilaya ya Makete mkoani Njombe umeendesha mafunzo kwa maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo  ya Jamii (wawezeshaji wa TASAF kwa Wilaya) kwa lengo la kwenda kufanya uhakiki kwa walemavu walioko kwenye Kaya za wanufaika wa TASAF


Mafunzo hayo yamefanyika ukumbi wa mji mdogo Iwawa Kata ya Iwawa kwa muda wa siku mbili tarehe 2-3 Novemba, 2022.


Zoezi la kuhakikia walemavu walipo kwenye Kaya zinazonufaika na TASAF limeanza tarehe 4 Novemba, 2022 na linatarajia kukamilika tarehe 6 Novemba, 2022, zoezi hilo linafanyika katika Kata zote 23 za Wilaya ya Makete.


Mwezeshaji katika mafunzo hayo ni Yassin Mkwepu Afisa kutoka TASAF Makao Makuu amesema kuwa TASAF imeandaa utaratibi wa kuhakiki Kaya zote zenye watu wenye ulemavu kupitia mikutano ya Vijiji/Mitaa/Shehia kwa usimamizi wa wawezeshaji kutoka mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa kuzingatia vigezo.


Pia Mkwepu ameeleza kuwa watu wenye ulemavu wanaohakikiwa ni wale ambao walijaziwa taarifa zao wakati wa zoezi la utambuzi wa Kaya Maskini.


Vigezo vya uhakikia vitazingatia watu wenye ulemavu wa Viungo, Ulemavu wa kuona, Ualbino, Ulemavu wa kusikia/kiziwi na ulemavu wa akili/ugonjwa wa akili.


Credit:maketedc.go.tz

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top