VERONICA ATOROKA KITUO CHA POLISI AKITUHUMIWA KWA WIZI

0

 

Polisi mtaani Kayole, Nairobi wameanzisha msako wa kumsaka mfungwa aliyetoroka akiwa katika Kituo cha Polisi cha Kayole.


Mfungwa huyo alikuwa anapelekwa kituoni humo akitokea katika Mahakama ya Makadara mnamo Jumatatu, Novemba 14, 2022.


Veronica Mutheu mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni mkazi wa Villa Embakasi alikuwa amekamatwa na polisi kwa wizi na kupelekwa katika Mahakama ya Makadara siku hiyo Jumatatu. Hata hivyo, maombi yalitolewa na kesi hiyo ilipangiwa kutajwa Jumatano, Novemba 16, 2022.


Mutheu alikuwa ameandamana pamoja na maafisa wawili wa polisi kwenye gari lililompeleka na kumrudisha kutoka mahakamani.


Waliporejea katika Kituo cha Polisi cha Kayole, maafisa hao wawili waliungana na wenzao watatu na mmoja wao alikuwa wa kutoka katika Kituo cha Polisi cha Hurlingham.


 Konstebo Wachira Daniel na Philip Kipsang waliokuwa ndani ya gari hilo pamoja na mfungwa huyo walishuka katika Kituo cha Polisi cha Kayole.


Kulingana na Wachira, mfungwa huyo alitoroka bila kujulikana karibu na lango la kituo cha polisi. “Konstebo Daniel Wachira ambaye alikuwa kwenye zamu aliwasindikiza wafungwa kortini akiwa na Maafisa wengine wawili katika gari la Usajili wa GK Nambari ya GKB Y hadi Mahakama ya Makadara. 


Faili ya kutoroka kwa mfungwa imefunguliwa na maafisa wote wameagizwa kuwa macho huku wananchi wakiombwa kutoa taarifa ya mahali popote Veronica ataonekana. 

ULITAZAMA VIDEO HII YA FURSA MTANDAONI? KAMA BADO BOFYA KUTAZAMA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top