WAHUKUMIWA MIAKA 120 JELA NA KUCHAPWA VIBOKO 48 KISA HIKI HAPA

0


Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka miaka 120 kwenda jela na kuchapwa viboko 48 kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, ingawa kila mshatakiwa amehukumiwa miaka 30 jela na viboko 12 kwa kila kosa, kwa makosa manne waliyoshtakiwa nayo, kila mshatakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 na viboko 12, kwa makosa yote kwa kuwa vifungo hivyo vitatumikiwa vyote kwa pamoja.

Hukumu ya kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2021 imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Samuel Maweda baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuiba mali mbalimbali zikiwamo fedha taslimu, simu, kompyuta mpakato ‘laptop’ pamoja na kujeruhi kwa kutumia panga.

Awali wakili wa Serikali Winfrida Ernest aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao, Emanuel Matulanya (20) Musa Soro (20) na Philipo Lucas (18) wanashtakiwa kwa makosa manne ya unyanganyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu namba 287 cha sheria ya adhabu.

Walipotakiwa kujitetea washtakiwa hao waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa la kwanza huku mshatiwa wa pili Musa Soro akiomba apunguziwe adhabau kwa kuwa ana mke na mtoto mmoja wanaomtegemea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top