WANANCHI WA KIJIJI CHA IKONDA WAKUBALI KUTIMIZA NDOTO ZA KUWA NA ZAHANATI

0

 

Wananchi wa Kijiji cha Ikonda Wilayani Makete mkoani Njombe wamejitokeza kwa wingi kufanya maandalizi katika kiwanja ambacho itajengwa zahanati ya kijiji hicho

 

Novemba 12,2022 wananchi hao wamefika katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya matayarisho ikiwemo kuchimba visiki na kung'oa miti iliyopo katika eneo hilo tayari kwa maandalizi ya ujenzi wa zahanati hiyo

Abson Kipene na Anjeline Mbilinyi ni wananchi wa kijiji hicho wakizungumza na mwandishi wetu katika eneo hilo la ujenzi wamesema wameupokea mradi huo kwa moyo mkunjufu na ndiyo maana wapo bega kwa bega na serikali ili kuhakikisha ujenzi huo wa zahanati unakamilika


Wamesema zahanati hiyo ikikamilika itawezesha wananchi hao kupata matibabu madogo madogo kwa haraka na kuepuka kwenda hospitali kupata matibabu hata ya magonjwa ambayo yangeweza kutibika katika ngazi ya zahanati


Upendo Sanga ni Katibu wa Kitongoji cha Luchala inapojengwa zahanati hiyo amesema ujenzi huo ameupokea kwa mikono miwili na uhitaji upo licha ya kuwa na hospitali kubwa kijijini hapo


Nancy Swai ni Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Tandala lakini pia ni Kaimu afisa mtendaji wa Kijiji cha Ikonda amesema mradi huo ni kwa ushirikiano na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) hivyo kuishukuru kwa wao kama kijiji kupata mradi huo


Amesema Kijiji hicho kina uhitaji wa zahanati kwa sasa hata kama kuna hospitali kwa kuwa sio kila matibabu yanapatikana katika hospitali kubwa hivyo magonjwa mengine yatatibiwa katika zahanati yao na pia itasaidia kuokoa muda


Diwani wa kata ya Tandala Daniel Hatanaka akizungumza eneo la tukio amesema wanaupokea kwa mikono miwili mradi huo na kuwaomba wananchi kujitokeza kufanya shughuli za maendeleo pale wanapohitajika kwa kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo kwa siku zijazo inaweza kuja kuwa kituo cha afya

TAZAMA VIDEO HII YA FURSA MTANDAONI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top