WANANFUNZI 500 WATOROKA SHULENI SIKU MOJA,DC AONYA WALIMU

0

 

Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo amesema katika wilaya hiyo ameshuhudia wanafunzi 500 wa shule moja wakitoroka masomo ndani ya siku moja ambapo amewaonya walimu wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi muda wa kuwa darasani kwani hali hiyo inachangia utoro

"Ni aibu kubwa shule moja siku moja ina watoro 500, imetokea katika wilaya hii na katika halmashauri hii", alisema Shimo" 

Shimo ametoa maagizo hayo kwa walimu wakati anaongea na walimu, viongozi wa kata na wananchi kwenye mamlaka ya mji mdogo Katoro baada ya kuona utoro uliokithiri kwenye wilaya hiyo huku serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya elimu kila siku. 

"Kwa mamlaka zote ambazo zinahusiana na elimu na bahati nzuri mdhibiti ubora yupo hapa, utoro wa namna hii kwa watumishi kutokuwa kwenye maeneo ya kazi, masaa na muda wa kazi  si jambo jema na ningeomba likome liachwe"

Mdhibiti mkuu ubora wa shule wilayani hapo Dismas Manyonyi amekiri kuwepo kwa utoro  wa walimu ambao  umeleta athari kubwa kwenye sekta ya  Elimu na kupelekea baadhi wanafunzi kupata mwanya wa kutohudhuria shuleni.

"Katika maeneo yangu imeonekana walimu wanafanya shughuli za bodaboda,  walimu wengine wanauza maduka ya bodhaa mbalimbali na wengine wana kuwa na shughuli mbalimbali za namna hiyo, kuna wengine tumewakuta mwaka unakwisha form two kwa mfano wanafanya mitihani mwalimu hajamaliza topic tatu  katika tisa sasa watoto wanaingia kwenye mtihani let say mtihani wa Physics, watoto wanaingia kwenye mtihani hawajamaliza topics tatu, sasa ujategemea watafanya nini? Moja kwa moja watafeli", alisema Manyonyi.

JE! UNAJUA UNAWEZA KUTENGENEZA KIPATO CHA ZIADA MTANDAONI? KAMA HUAMINI TAZAMA VIDEO HII.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top