WATANZANIA WENGINE WAJIINGIZA KUTAPELIWA TENA LEO NA 20GB

0

kumekuwepo Ujumbe ukisambazwa kwa wingi mtandaoni hasa whatsapp kuhusu Ofa ya 20GB kutoka mitandao yote ambayo imeelezwa kuwa ni kusherekea maadhimisho ya mitandao ya simu nchini.


Ujumbe huo unaeleza kuwa washiriki wabofye link/kiungo kilichoambatanishwa na ujumbe huo ili kupata 20GB kwenye line zao na kwamba Ofa hiyo itakoma tarehe 15 Novemba 2022,Swali ni Je! ni kweli unaweza kupata OFA hiyo?

NINI KINACHOFANYIKA?
Kinachofanyika ni kwamba kuna wajanja kwa kuwa wanajua watanzania wengi hawajui masuala ya mitandao,wanatengeneza link kama hizo za ofa kisha wanakwambia bofya kuendelea ukibofya kuendelea utakutana na survey au utafiti wa kingereza ambayo umeundwa kama tangazo hivyo kadri unavyoendelea kubofya ndivyo unavyowatengenezea pesa wenzako.

NINI NIKIFANYE NIKIPOKEA UJUMBE WA OFA?
Hakikisha unaepuka ofa za bure? hasa katika mitandao ambayo inakutaka ubofye link/kiunge kinachoambatanishwa sababu hujui wanamalengo gani juu yako na taarifa zako utakazo shirikisha kwao,Zaidi naomba utazame video hii nimekupa ujanja kujua ni matapeli au la! KARIBU.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top