Watoto wawili wa umri wa miaka minne na miwili wamelazwa hospitalini baada ya kula chakula kisichofaa.
Duru zimearifu watoto hao walipikiwa nyama ya kinyonga waliyokula na kupata matatizo ya kiafya.
Mama ya wawili hao alisema mwanawe wa miaka saba ndiye alikuwa nyumbani na kuamua kuwapa watoto hao nyama hiyo.
"Ndugu yao wa miaka saba aliwapikia viazi na nyama hiyo ya kinyonga," alisema huku akihuzunika na yale yaliyofanyika.
Watoto hao sasa wamelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Molo ambapo imearifiwa wameweza kupokea matibabu vizuri.
"Nimeweza kutembea katika hospitali kuwajulia hali watoto hao wawili kutoka Sirikwa, Nyakinyua na wamepokea matibabu vizuri. Wataweza kuruhusiwa kuenda nyumbani hivi karibu," alisema mwanasiasa Leonard Bor wa Kuresoi.
Wakazi wengi wamepinga ripoti kwamba kia hicho kilitokana na ukosefu wa chakula wakisema huenda ni hali tu ya utoro wa aliyewapikia nyama hiyo.
"Yaani wanataka kutuambia eti Kuresoi kuna shida ya njaa. Hakuna kitu kama hiyo, nimekataa. Hapa ni shida tu ya ulezi," mwanamtandao mmoaj alisema.
Chanzo: TUKO.co.ke