Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru Washitakiwa 24 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Askari Polisi G 4200 Koplo Garlus Mwita Wilayani Ngorongoro baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha nia ya kutoendelea na kesi hiyo.
Kesi hiyo ilipangwa leo kwa ajili ya kutajwa ambapo kati ya Washtakiwa hao 24, kumi ni Madiwani pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngorongoro, Nderango Laizer.
Mbele ya Hakimu Mkazi Herieth Mhenga, Jamhuri katika kesi hiyo ya mauaji namba 9/2022 iliwakilishwa na Wakili Upendo Shemkole ambaye aliieleza Mahakama shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni njama ya mauaji, ambapo wanadaiwa kupanga njama ya kuua Maafisa wa Serikali na Polisi watakaoshiriki zoezi la kuweka mipaka pori tengefu la Loliondo.
Kosa la pili ni mauaji ambapo wanadaiwa Juni 10, 2022 eneo la Ololosokwan, Ngorongoro kwa nia ovu walisababisha kifo G 4200 cha Koplo Garlus Mwita.
USISAHAU KUTAZAMA VIDEO HII ITAKUSAIDIA KUBADILI MTAZAMO WAKO