WILAYA KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI 3, ZATOA MISAADA KWA WATU 9 WENYE ULEMAVU WILAYA YA MKOANI.

Hassan Msellem
0

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mheshimiwa Khatib Juma Mjaja, amewaomba wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutokuwaficha ili waweze kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu na taaluma mbali mbali.

Ametoa ombi hilo wakati akikabidhi vifaa kwa watu wenye ulemavu huko, amesema ulemavu ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo wazazi hawana budi kuikubali na kuipokea mitihani hiyo ili watoto wenye ulemavu wajihisi kama watoto wengine wasio na ulemavu.

"Hakuna mtu anayeomba azaliwe na ulemavu lakini inakuwa ni mtihani, Kwahivyo kubwa kwenye mtihani kinachotakiwa ni kushukuru lakini pia kuupokea na kuupokea ni kuhisi mtoto wako mwenye ulemavu ni sawa na watu watoto wengine na ukaweza kumtoa ili aweze kupatiwa haki zake zote za msingi anazihitaji ikiwemo elimu" DC Mjaja

Aidha mkuu huyo, amempongeza Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, kutokana na juhudi zake kuwafikia watu wenye ulemavu na kuweza kuwasaidia mahitaji yao mbali mbali.

 Kwa upande wake afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo taasisi ya vichwa vikubwa na mgongo wazi, taasisi ya Nuru Foundation pamoja bandari kwa moyo wao wakujitolea kuwasaidia watu wenye ulemavu.

"Kuwasaidia watu wenye ulemavu ni suala mtambuka sio kwamba tu linahusiana na ofiisi ya mkuu wa Wilaya tunafahamu kuwa watu wenye ulemavu wanahitaji huduma zote kama wanavyohitaji watu wengine, kwahivyo tunaomba taasisi ambazo zinatoa huduma kwenye jamii ikiwemo watu wa bandari watu wa barabara katika utekelezaji wa majukumu yao wazingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu kwasababu sote ni walemavu watarajiwa" alisema 

"Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mheshimiwa Khatib Juma Mjaja, amewaomba wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutokuwaficha ili waweze kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu na taaluma mbali mbali.

Ametoa ombi hilo wakati akikabidhi vifaa kwa watu wenye ulemavu huko, amesema ulemavu ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo wazazi hawana budi kuikubali na kuipokea mitihani hiyo ili watoto wenye ulemavu wajihisi kama watoto wengine wasio na ulemavu.

"Hakuna mtu anayeomba azaliwe na ulemavu lakini inakuwa ni mtihani, Kwahivyo kubwa kwenye mtihani kinachotakiwa ni kushukuru lakini pia kuupokea na kuupokea ni kuhisi mtoto wako mwenye ulemavu ni sawa na watu watoto wengine na ukaweza kumtoa ili aweze kupatiwa haki zake zote za msingi anazihitaji ikiwemo elimu" DC Mjaja

Aidha mkuu huyo, amempongeza Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, kutokana na juhudi zake kuwafikia watu wenye ulemavu na kuweza kuwasaidia mahitaji yao mbali mbali.

Mohammed Issa Makame, mwenye ulemavu wa ualbino akipokea shilingi laki 2 na elfu thelathini kwa ajili ya mtaji wa kuchuzia Samaki.

Kwa upande wake afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo taasisi ya vichwa vikubwa na mgongo wazi, taasisi ya Nuru Foundation pamoja bandari kwa moyo wao wakujitolea kuwasaidia watu wenye ulemavu.

"Kuwasaidia watu wenye ulemavu ni suala mtambuka sio kwamba tu linahusiana na ofiisi ya mkuu wa Wilaya tunafahamu kuwa watu wenye ulemavu wanahitaji huduma zote kama wanavyohitaji watu wengine, kwahivyo tunaomba taasisi ambazo zinatoa huduma kwenye jamii ikiwemo watu wa bandari watu wa barabara katika utekelezaji wa majukumu yao wazingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu kwasababu sote ni walemavu watarajiwa" alisema 

Nao baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ulemavu wamezishukuru taasisi hizo kwa misaada waliowapatia na kuahidi kuyatunza na kuifanyia kazi ili iweze kufikia lengo la kutolewa kwake.

Aidha katika utoaji wa misaada hiyo, taasisi hizo zimetoa msaada wa mkoba, kikotoo, Sabuni pamoja na fedha za matumizi kwa Kijana  Amani Maabadi Maalim, Mkaazi wa Michenzani ambaye aliacha kusoma mwaka 2018 Kutokana na hali ngumu ya maisha inayoikabili familia yake.

"Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya huyu kijana alipasi michepuo darasa na kidato cha nne na kufanikiwa kwenda form five lakini alilazimika kuacha kutokana na hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili kwani mama yake hakuwa na uwezo wakumsomesha baada ya kutumia fedha nyingi kimuuguza mdogo wake ambaye anaulemavu wa akili na viungo, lakini tulipambana kumtafutia wahisani na hatimae Mungu amejaalia tumefanikiwa na kwasasa ataendelea na masomo katika Skuli ya Sekondari ya Madungu Chake Chake" Alisema afisa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed.

Amani Maabadi Maalim, akikabidhiwa mkoba na Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, kwa ajili ya kurudi masomoni.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Vitimwendo, fedha taslim shilingi 23'0000, Godoro, mkoba ya shule, Pampus pamoja na Miwani.

Misaada hiyo imetolewa na Ofisi ya watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Kwa kushirikiana na taasisi ya Vichwa vikubwa na mgongo wazi, taasisi ya Nuru Foundation pamoja na Mamlaka ya Bandari Mkoani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top