AJALI NYINGINE YAUA MUME NA MKE

0

 Wanandoa wawili Tumaini John (41) aliyekuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo Maruku katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, na mme wake Geofrey John (42) mfanyabiashara, wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongana na basi la kampuni ya Happy Nation.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Kamanda wa polisi mkoani Kagera  William Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo ilitokea  saa 5:30 asubuhi katika barabara itokayo Bukoba kwenda Biharamulo eneo la Ijuganyondo

Amesema basi hilo aina ya Youtong liligongana na pikipiki hiyo aina ya SANLG na kusababisha vifo vya watu hao

"Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva mmoja wa pikipiki aliyekuwa amepakia magunia ya mkaa kuisukuma pikipiki waliyokuwa wamepanda watu hao na kusababisha pikipiki yao kukosa mwelekeo na hivyo kugongana na basi hilo la Happy Nation, na kusababisha vifo vyao papo hapo" amesema Mwampaghale.

Chanzo;Muungwana

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top