ALIYEDAI NI MSHAURI WA RAIS SAMIA AKAMATWA NA POLISI

0

 OLISI Mkoa wa Tanga imemkamata mkazi wa Ukonga, Dar es Salaam, Zainabu Kagoso (50), akidaiwa kujitambulisha kuwa ni mshauri wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi na kutumia njia hiyo kutapeli ofisi za serikali na maeneo mbalimbali wilayani Kilindi.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mtu huyo mara baada ya kukamatwa pia alidai ni ofisa usalama yupo Tanga kwa kazi maalum, ambapo amekuja kufuatilia kazi alizotumwa.

"Tumemkamata mtu mmoja mwanamke mkazi wa Ukonga Dar es Salaam, amekuja mkoani Tanga hasa wilaya ya Kilindi, akiwa anaenda ofisi mbalimbali za serikali, akidai yeye ni ofisa usalama wa Taifa na amekuja kwa kazi maalum na kwamba yeye ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi, amekuja kuangalia kazi mbalimbali aliyotumwa, " amesema Kamanda Mwaibambe.
CLICK CLICK CLICK VIDEO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top