BUNGE LAGEUKA MAWINDO YA DADA POA

0

Biashara ya haramu ya ngono imekuwa ngumu kudhibiti katika nchi mbalimbali na nyingine zikienda mbali sana sasa mara huko nchini Kenya warembo waanza kuwamezea mate wabunge wakikaa nje ya lango kuu ya Bunge kuona namna ya wabunge kunasa katika penzi lao.


Kwa mujibu wa gazeti la Nation Jumapili, walinda lango katika bunge wamekuwa na kibarua kila uchao kutokana na warembo wanaofika kuwatafuta wabunge.


Duru ziliarifu gazeti hilo kwamba kuna msukumano katika lango kila siku huku vipusa waliovalai kwa namna ya kuanika mapaja nje wakijaa hapo.


"Tunashindwa namna ya kuwakabili kwa sababu hujui kwa ukamilifu wanajuana vipi na mheshimiwa," alisema mlinzi mmoja na gazeti hilo. 


Huku wakihofia kuwakasirisha waheshimiwa, walinzi wamelazimika kutafuta mbinu za kuwakaribisha vipusa hao. 

TAZAMA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPA ITAKUSAIDIA


Gazeti hilo lilisema warembo sasa wamekuwa wakiwekwa kwenye chumba kimoja karibu na lango kusubiri mheshimiwa wanayemtaka.


Kina dada wa umri mdogo wamekuwa wakimezea mate waheshimiwa na mara nyingi hujipata wamekuwa kitoweo chao. 


Pesa na magari ya kifahari sawa na ziara za hapa na pale zimekuwa ndio chambo kwa vipusa hawa waliobarikiwa na urembo lakini wakakosa maadili. 

JE! UNAAMINI KAZI ZA MTANDAAONI KWA ASILIMIA NGAPI? BOFYA VIDEO HII

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top